Tuesday, August 31, 2010

MALE SHIRTS FROM KOKOLILO


TRADITIONAL WEDDING DRESS FROM KOKOLIKO

WADAU HILI NI GAUNI LA HARUSI LILILOTENGENEZWA NA KOKOLIKO KWA KUTUMIA MATERIALS YA KITENGE AMBAYO YANAPATIKANA HAPA KWETU.KWA PICHA NYENGINE NTAWAPOSTIA PUNDE.KUWENI NA SUBIRA

Monday, August 30, 2010

BAZEE FROM KOKOLIKO COLLECTION


WADAU HIZI NI BAADHI YA KAZI ZA DADA AISHA KISOKI AMBAYE ANAPATIKANA KUPITIA NAMBA +255713510530.

KOKOLIKO DESIGNS BY AISHA KISOKI


WADAU HUYU NI DADA AISHA KISOKI AKA MAMA WA SOFIA PRODUCTION AMBAYE ANASHUGHULIKA NA UCHUKUAJI WA VIDEO (VIDEO PRODUCTION) NA VILEVILE NI MBUNIFU WA MITINDO YA NGUO KWA KUTUMIA RASILIMALI ZA KITANZANIA KAMA BATIKI.VITENGE,NA MATERIALS NYENGINE.
NILIPATA BAHATI YA KUBADILISHANA NAE MAWAZO KUHUSU FANI NZIMA YA  MITINDO NA KUNIAHIDI KAMA ATAFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KWENYE FANI HII YA MITINDO  KWA KUTOA HAMASA KWA WATANZANIA KUTUMIA NGUO ZILIZOTENGENEZWA NA VITAMBAA VYETU.
ANABUNI KWA KUTUMIA MATERIALS YOTE YA KITANZANIA KAMA BATIKI,KIKOI,MASAI.PIA ALINIONYESHA BAADHI YA KAZI ZAKE AMBAZO TAYARI ZIKO NDANI YA STOCK KWA AJILI YA KUJIPANGA NA ONYESHO .
KWA TAARIFA ZAIDI ZA MITINDO YAKE NA ONYESHO ANALOKUSUDIA KULIFANYA  NITAWAPA TAARIFA BAADAYE MARA BAADA YA KUKAMILISHA MCHAKATO  MZIMA. KWA WALE AMBAO WATAPENDA KAZI ZAKE NA KUTAKA KUNUNUA NITAWAPA CONTACT ZAKE. ILA KWA SASA ANAPATA TANGA INDIA STREET KARIBU NA ECKERNFORDE SECONDARY AU TEXAS PUB NDANI YA OFISI YA SOFIA PRODUCTION.

Tuesday, August 24, 2010

MAHOJIANO NA DEUTSCHE WELLE

NAPENDA KUWAJULISHA WAPENZI WA BLOG YANGU KUWA NILIKUWA NA INTERVIEW NA SAUMU MWASIMBA WA DEUTSCHE WELLE UJERUMANI JUU YA MATUMIZI YA VIPODOZI VYA ASILI KAMA LIWA NA HABBAT SAWDA AMBAZO NILISHAWAHI KUPOST KWENYE HII BLOG.KIPINDI KITARUSHWA SIKU YA IJUMAA ASUBUHI SAA KUMI NA MBILI KWA SAA ZA AFRICA MASHARIKI KUPITIA RADIO ZA FM AMBAZO ZINARUSHA MATANGAZO YA RADIO HIYO

Monday, August 23, 2010

HAPPY BIRTHDAY-HALLE BERRY

MWANAMITINDO NA MCHEZA SINEMA HALLE BERRY HATIMAYE AMETIMIZA MIAKA 44.BLOG YA http://www.abdallahmasoud.blogspot.com/ INAKUOMBEA MUNGU UPATE 44 MENGINE.INSHALLAH AMIN

ONE SHOULDER DRESSES



MODEL OF THE DAY

LAURNY HILL

JANELLE MONAE HAIR STYLE

SEXIEST BALD STYLE

                                            1.MICHAEL  JORDAN.
2.JAMMIE FOX.

3.COMMON.

4.TYRESE.


DISCO DANCER

MAMBO YA  MITHUN CHAKRABOTHY

RAIS MTARAJIWA WA HAITI

WYCLEFF JEAN

Saturday, August 14, 2010

DU'AA ANAZOZIHITAJI MUISLAMU KATIKA RAMADHANI

1.Du'aa ya kwenda Msikitini
اللّهُـمَّ اجْعَـلْ فِي قَلْبـي نُوراً ، وَفي لِسَـانِي نُوراً، وَفِي سَمْعِي نُوراً, وَفِي بَصَرِيِ نُوراً, وَمِنْ فََوْقِي نُوراً , وَ مِنْ تَحْتِي نُوراً, وَ عَنْ يَمِينيِ نُوراَ, وعَنْ شِمَالِي نُوراً, وَمْن أَماَمِي نُوراً, وَمِنْ خَلْفيِ نُوراَ, واجْعَلْ فِي نَفْسِي نُوراً, وأَعْظِمْ لِي نُوراً, وَعظِّمْ لِي نُوراً, وَاجْعَلْ لِي نُوراً, واجْعَلنِي نُوراً, أللَّهُمَّ أَعْطِنِي نُوراً, واجْعَلْ فِي عَصَبِي نُوراً, وَفِي لَحْمِي نُوراً, وَفِي دَمِي نُوراً وَفِي شَعْرِي نُوراً, وفِي بَشَرِي نُوراً (أَللَّهُمَّ اجِعَلْ لِي نُوراً فِي قّبْرِي وَ نُوراَ فِي عِظاَمِي) (وَزِدْنِي نُوراً, وَزِدْنِي نُوراَ , وَزِدْنِي نُوراً) (وَهَبْ لِي نُوراً عَلَى نُوراً )

Allaahumma-j-'al Fiy Qalbiy Nuuraa, Wa fiy Lisaaniy Nuuraa Wa fiy Sam'iy Nuuraa, Wa Fiy Baswariy Nuuraa, Wa Min Fawqiy Nuuraa, Wa Min Tahtiy Nuuraa, Wa 'An Yamiiniy Nuuraa, Wa 'An Shimaliy Nuuraa, Wa Min Amaamiy Nuuraa, Wa Min Khalfiy Nuuraa, Waj-'al Fiy Nafsiy Nuuraa, Wa A'adhwim Liy Nuuraa, Wa 'Adhwim Liy Nuuraa, Waj-'al-Liy Nuuraa, Waj-alniy Nuuraa, Allaahuumma A'atwiniy Nuuraa, Waj'al fiy 'Aswabiy Nuuraa, Wa fiy Lahmiy Nuuraa, Wa fiy Damiy Nuuraa Wa fiy Sha'ariy Nuuraa, Wa fiy Bashariy Nuuraa. Allaahumma-j'al liy Nuuran fiy Qabriy, Wa Nuuran Fiy 'Idhaamiy, Wazidniy Nuuraa, Wazidniy Nuuraa, Wazidniy Nuuraa, Wahab liy Nuuran 'Alaa Nuuraa.


“Ewe Mwenyezi Mungu, Weka katika moyo wangu nuru, na katika ulimi wangu nuru, na katika masikio yangu nuru, na katika macho yangu nuru, na juu yangu nuru, na chini yangu nuru, na kuliani kwangu nuru, na kushotoni kwangu nuru, na mbele yangu nuru, na nyuma yangu nuru, na Weka katika nafsi yangu nuru, na Nifanyie kubwa nuru, na Nifanyie nyingi nuru, na Uniwekee mimi nuru, na Nifanyie mimi nuru, Ewe Mwenyezi Mungu Nipe nuru, na Uweke katika mishipa yangu nuru, na katika nyama yangu nuru, na katika damu yangu nuru, na katika nywele zangu nuru, na katika ngozi yangu nuru, (Ewe Mwenyezi Mungu Niwekee nuru katika kaburi langu, na nuru katika mifupa yangu) (Na Unizidishie nuru, na Unizidishie nuru, na Unizidishie nuru) (na Unipe nuru juu ya nuru ) .


2.Du'aa ya kuingia Msikitini

أَعُوذ باللهِ العَظيـم وَبِوَجْهِـهِ الكَََرِِيـمِ وَسُلْطـانِهِ القََدِيـمِ مِنَ الشّيْـطانِ الرَّجِـيمِ،[ بِسْـمِ الله، وَالصَّلاةُ] [وَالسَّلامُ عَلى رَسولِ الله]، اللّهُـمَّ افْتَـحْ لي أَبْوابَ رَحْمَتـِكَ

A'udhu BiLLahil-'Adhwiym Wabiwaj-hihi-l-Kariym Wasul-twaanihi-l-Qadiym Mina-shaytwaanir-rajiym. BismiLLahi Was-Swalaatu Wassalaamu 'Alaa RasuliLLah. Allaahummaf-tah liy Abwaaba Rahmatika.

“Najilinda na Mwenyezi Mungu Aliye Mtukufu, na kwa uso Wake, Mtakatifu, na kwa utawala Wake wa kale, kutokana na shetani aliyeepushwa na rehma za Mwenyezi Mungu, (Kwa Jina la Mwenyezi Mungu na rehma) (Na amani zimfikie Mtume wa Mwenyezi Mungu ) Ewe Mwenyezi Mungu Nifungulie milango ya rehma Zako"

3.Du'aa ya kutoka Msikitini

بِسمِ الله وَالصّلاةُ وَالسّلامُ عَلَى رَسولِ الله، اللّهُـمَّ إِنّـي أَسْأَلُكَ مِـنْ فَضْـلِك، اللّهُـمَّ اَعْصِمْنـي مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجـيم

Bismillahi Was-Swalaatu Was-Salaamu 'Alaa RasuliLLah, Allaahumma Inniy As-aluka Min Fadhlika Allaahumma A'aswimniy Minash-shaytaani-rajiym.

“Kwa Jina la Mwenyezi Mungu na rehma na amani zimfikie Mtume wa Mwenyezi Mungu, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba katika fadhila Zako, Ewe Mwenyezi Mungu najilinda kutokana na shetani aliyeepushwa na rehma Zako (aliyelaaniwa )

4.Du'aa ya Qunuut ya Witr
اللّهُـمَّ اهْـدِنـي فـيمَنْ هَـدَيْـت، وَعـافِنـي فـيمَنْ عافَـيْت، وَتَوَلَّـني فـيمَنْ تَوَلَّـيْت ، وَبارِكْ لـي فـيما أَعْطَـيْت، وَقِـني شَرَّ ما قَضَـيْت، فَإِنَّـكَ تَقْـضي وَلا يُقْـضى عَلَـيْك ، إِنَّـهُ لا يَـذِلُّ مَنْ والَـيْت، [ وَلا يَعِـزُّ مَن عـادَيْت ]، تَبـارَكْـتَ رَبَّـنا وَتَعـالَـيْت.

Allaahummah-diniy fiyman Hadayta , Wa 'Aafiniy fiyman 'Aafayta, Watawallaniy fiyman Tawallayta, Wabaarik liy fiymaa A'atwayta, Waqiniy Sharra Maa Qadhwayta, Fainnaka Taqdhwiy Walaa Yuq-dhwa 'Alayka, Innahu Laa yadhillu mawwaalayta, Walaa Ya'izzu man 'Aadayta, Tabaarakta Rabbana Wa Ta'aalayta.

“Ewe Mwenyezi Mungu Niongoze pamoja na Uliowaongoza, na Unipe afya njema pamoja na Uliowapa afaya njema, na Nifanye kuwa ni mpenzi Wako pamoja na Uliowafanya wapenzi na Nibariki katika Ulichonipa na Nikinge na shari ya Ulilolihukumu kwani Wewe Unahukumu wala Huhukumiwi. Hakika hadhaliliki Uliyemfanya mpenzi (wala hatukuki Uliyemfanya adui ) Umetakasika Ewe Mola wetu na Umetukuka

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِرِضـاكَ مِنْ سَخَطِـك، وَبِمُعـافاتِـكَ مِنْ عُقوبَـتِك، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْـك، لا أُحْصـي ثَنـاءً عَلَـيْك، أَنْـتَ كَمـا أَثْنَـيْتَ عَلـى نَفْسـِك

Allaahumma Inniy A'udhu Biridhwaaka Min Sakhatwika, Wabimu'aafaatika min 'Uquubatika, Wa A'udhu Bika Minka, Laa Uhswiy Thanaan 'Alayka, Anta Kamaa Ath-nayta 'Alaa Nafsika.
“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwa radhi Zako kutokana na hasira Zako na kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako, na najilinda Kwako kutokana na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa Zako, Wewe ni kama Ulivyojisifu Mwenyewe”

اللّهُـمَّ إِيّـاكَ نعْـبُدْ، وَلَـكَ نُصَلّـي وَنَسْـجُد، وَإِلَـيْكَ نَسْـعى وَنَحْـفِد، نَـرْجو رَحْمَـتَك، وَنَخْشـى عَـذابَك، إِنَّ عَـذابَكَ بالكـافرين ملْحَـق. اللّهُـمَّ إِنّا نَسْتَعـينُكَ وَنَسْتَـغْفِرُك، وَنُثْـنـي عَلَـيْك الخَـيْرَ، وَلا نَكْـفُرُك، وَنُـؤْمِنُ بِك، وَنَخْـضَعُ لَكَ وَنَخْـلَعُ مَنْ يَكْـفرُك
Allaahumma Iyyaaka Na'abud Walaka Nuswalliy Wanasjudu, Wa-Ilayka Nas'aa Wanahfidu, Narju Rahmataka, Wanakhsha 'Adhaabaka, Inna 'Adhaabaka Bil-Kaafiriyna Mulhaqq. Allaahumma Innaa Nasta'iynuka Wanastaghfiruka, Wanuthniy 'Alaykal-khayra, Walaa Nakfuruka, Wanu-uminu Bika, Wanakhdhwa'u Laka, Wanakhla'u Man Yakfuruka.

“Ewe Mwenyezi Mungu, Wewe tu Ndiye tunaekuabudu, na Kwako tunaswali na tunasujudu, na Kwako tunakimbilia na tunakutumikia, tunataraji rehema Yako na tunaogopa adhabu Yako, kwani adhabu Yako hakuna shaka kuwa makafiri itawifikia. Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakutaka msaada na tunakutaka msamaha na tunakusifu kwa kheri na wala hatukukufurishi na tunakuamini Wewe, na tunakunyenyekea na tunamuepuka anaekukufuru”
Dua baada ya salamu katika swala ya Witri (Mwisho kabisa baada ya kumaliza Swalah yote na sio kila baada ya Rakaa mbili au nne)

سُـبْحانَ المَلِكِ القُدّوس
Subhaanal-Malikul-Qudduus
“Ametakasika Mwenyezi Mungu Mfalme, Mtakatifu"
(mara tatu)
(Kisha unavuta kwa sauti )

ربِّ الملائكةِ والرّوح

Hul-Malaaikati War-Ruuh
“Ewe Mola wa malaika na wa Jibriil”

5.Du'aa ya wakati wa kufungua Swawm

ذَهَـبَ الظَّمَـأُ، وَابْتَلَّـتِ العُـروق، وَثَبَـتَ الأجْـرُ إِنْ شـاءَ اللهُ
Dhahabadh-Dhwama-u Wabtallatil-'Uruuq,, Wathabbatal-Ajru Insha-Allaah.
“Kiu kimeondoka na mishipa imelainika, na yamethibiti malipo Mwenyezi Mungu Akipenda”
Imepokelewa kutoka kwa Abdillahi bin Amr bin Al Ass رضي الله عنه amesema: ‘Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu “Aliyefunga wakati wa kufuturu kwake ana Du'aa isiyorudishwa”

اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ بِرَحْمَـتِكَ الّتي وَسِـعَت كُلَّ شيء، أَنْ تَغْـفِرَ لِي

Allaahumma Inniy As-aluka Birahmatikal-latiy Wasi'at Kulla Shay'in An Taghfiraliy.
“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba kwa rehma Zako ambazo zimeenea kila kitu, Unisamehe”

6.Du'aa kabla ya kula
Atakapo kula mmoja wenu chakula basi aseme:
بِسْمِ الله
Bismillahi
“Kwa jina la Mwenyezi Mungu"
Na akisahau mwanzo wake basi aseme:
بِسْمِ اللهِ في أَوَّلِهِ وَآخِـرِهِ
Bismillahi Fiy Awwalihi Wa Aakihirihi

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo Wake na mwisho Wake”
Yeyote ambae Mwenyezi Mungu Amemruzuku chakula aseme:

اللّهُـمَّ بارِكْ لَنا فيهِ وَأَطْـعِمْنا خَـيْراً مِنْـهُ
Allaahumma Baarik Lana Fiyhi Wa Atw'imna Khayran minhu.
“Ewe Mwenyezi Mungu Tubariki katika chakula hichi na Tulishe bora kuliko hichi "
Na yeyote ambae Amemruzuku maziwa basi aseme:
اللّهُـمَّ بارِكْ لَنا فيهِ وَزِدْنا مِنْهُ
Allaahumma Baarik Lana Fiyhi Wazidna Minhu
“Ewe Mwenyezi Mungu Tubarikie kinywaji hichi na Utuzidishie”

7.Du'aa ya baada ya kula
الْحَمْـدُ للهِ الَّذي أَطْعَمَنـي هـذا وَرَزَقَنـيهِ مِنْ غَـيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلا قُوَّةٍ
Alhamduli-Llahi-lladhiy Atw'amaniy Haadhaa Warazaqaniyhi Min Ghayri Hawlim-Minniy Walaa Quwwatin.
“Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu Ambaye Amenilisha mimi chakula hichi na Akaniruzuku pasina uwezo wangu wala nguvu zangu”

الْحَمْـدُ للهِ حَمْـداً كَثـيراً طَيِّـباً مُبـارَكاً فيه، ]غَيْرَ مَكْفِيٍّ[ وَلا مُوَدَّعٍ وَلا مُسْتَغْـنىً عَنْـهُ رَبُّـنا
AlhamduliLLahi Hamdan Kathiyran Twayyiban Mubaarakan Fiyhi, Ghayra Mukfiyyi Walaa Muwadda'iw- Walaa Mustaghna 'Anhu Rabbunaa.
“Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, sifa nyingi nzuri, zenye baraka ndani yake, zisizo toshelezwa wala kuagwa, wala kutoshwa nazo mtu. Ewe Mola wetu”


8.Du'aa ya mgeni kumuombea aliyemkaribisha chakula
اللّهُـمَّ بارِكْ لَهُمْ فيما رَزَقْـتَهُم، وَاغْفِـرْ لَهُـمْ وَارْحَمْهُمْ
Allahumma Baarik Lahum Fiyma Razaq-tahum Waghfir-lahum War-ham-hum.
“Ewe Mwenyezi Mungu Wabariki katika Ulichowaruzuku na Uwasemehe na Uwarehemu"

9.Du'aa ya kumuombea aliyekupa kinywaji au anayetaka kukupa
اللّهُـمَّ أَطْعِمْ مَن أَطْعَمَني، وَاسْقِ مَن سَقانِي
Allaahumma Atw'im Man Atw'amaniy Wasqi Man Saqaaniy.

“Ewe Mwenyezi Mungu Mlishe aliyenilisha na Mnyweshe aliyeninywesha"

10.Du'aa ya kumuombea uliyefuturu/futari kwake
أَفْطَـرَ عِنْدَكُم الصّـائِمونَ وَأَكَلَ طَعامَـكُمُ الأبْـرار، وَصَلَّـتْ عَلَـيْكُمُ الملائِكَـة
Aftwara 'Indakumu-Swaaimuna Wa Akala Twa'aamakumul-Abraar, Waswallat 'Alyakumul-Malaaikah.
“Wafuturu kwenu waliofunga na wale chakula chenu watu wema, na wawaombee rehema malaika”

11.Du'aa ya aliyealikwa chakula lakini akawa amefunga
Akialikwa mmoja wenu aitike mwito, akiwa amefunga basi awaombee Du'aa na kama hakufunga basi ale
Anachosema aliyetukanwa hali ya kuwa amefunga
إنِّي صَائِمٌ , إنِّي صَائِمٌ”
Inniy Swaaimun Inniy Swaaimun

“Hakika mimi nimefunga, hakika mimi nimefunga"







Friday, August 6, 2010

TOP DESIGNERS

TOP DESIGNERS IN THE WORLD STEFFANO GABBANA AND DOMENICO DOLCE OF DOLCE &GABBANA LABEL

LADY IN RED

NAEEM KHAN-FALL 2010